#HABARI: Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Yohana John (40), Mkazi wa Kijiji cha Imbilili wilayani Babati, mkoani Manyara, amefariki dunia Januari 28, 2025, kwa kujinyonga.
Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa marehemu, Merian John, amekiri kuwa mwanae alikuwa akisumbuliwa na tatizo la afya ya akili, jambo linalodaiwa kuwa limechangia kutokea kwa tukio hilo.
Aidha, amesema kuwa kabla ya kifo chake, Yohana alikuwa akionesha tabia zisizo za kawaida, ikiwemo kwenda kukagua kaburi na kueleza sehemu aliyotamani azikwe.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Imbilili, Marcel Krisent, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.
Aidha, amewataka wananchi kuwa karibu na watu wanaokabiliwa na changamoto za afya ya akili, ili waweze kupata msaada wa mapema na kuzuia matukio kama haya kujirudia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.