Dar es Salaam. Leo Jumamosi, Saa 7:00 usiku, Yanga imemtambulisha Buba Jammeh kuwa mchezaji wake mpya ikimnasa kutoka Interclube ya Angola kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo ana umri wa miaka 24 na ni raia wa Gambia ingawa pia ana uraia wa Angola ambako ameishi kwa miaka mitano.

Hadi anajiunga na Yanga, Jammeh ameitumikia Interclube katika michezo saba yote ikiwa ya Ligi Kuu Angola na kufunga bao moja.

Mchezaji huyo anamudu kucheza winga za pande zote kwa vile ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha akibebwa na kasi pamoja na chenga za maudhi.

Jammeh anayemudu pia kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, ana uzito wa kilo 60 na urefu wa sentimita 177.

Jammeh anakuwa mchezaji wa pili raia wa Gambia kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, wa kwanza akiwa ni Lamine Jarju aliyepo Singida Black Stars.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *