
Waziri huyo ameviambia vyombo vya habari vya shirika la RND kwamba itakuwa kosa kama watakuwa wanaiangalia Ikulu ya White House kama sungura anavyomtazama nyoka. Na kuonya kwamba kufanya hivyo watakuwa wanapoteza mwelekeo wa kile wanachopaswa kufanya, kuwa na mamlaka zaidi na kujitegemea.Ameongeza kwa kusema Rais wa Marekani, Donald Trump, anategemea hali ya kutokuwa na uhakika na hofu ili kufanikisha malengo yake. Pistorius amehimza kutokukubali kutishwa, akisisitiza upinzani wa serikali za Ulaya dhidi ya hatua ya Trump kusukuma kwa nguvu ajenda ya Marekani kuchukua udhibiti wa Greenland, eneo lenye kujitegemea kwa sehemu na linalomilikiwa na Denmark.