Uhispania haitashiriki katika mashindano ya Eurovision “ikiwa Israel itaendelea kushiriki katika tamasha la muziki huku mauaji ya watu wengi huko Gaza yakiendelea,” shirika la utangazaji la RTVE limetangaza leo Jumanne, Septemba 16.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Ikiwezekana, Uhispania itajiunga na Ireland, Slovenia, Iceland, na Uholanzi, ambazo tayari zimeonyesha kwamba hazitatuma mwakilishi kwenye toleo lijalo ikiwa Israel itashiriki. 

Hata hivyo, Uhispania ni nchi ya kwanza kati ya zile zinazoitwa “Big Five”, ambayo ni pamoja na wachangiaji wakuu wa shindano hilo (Uhispania, Uingereza, Ufaransa, Italia na Ujerumani), kutishia kususia.

Waziri wa Utamaduni wa Uhispania Ernest Urtasun amesema siku ya Jumatatu kwamba Uhispania haipaswi kushiriki katika toleo hili la shindano ikiwa Israel itashiriki? Nchi nyingine tayari zimetangaza kwamba zitasusia.

“Lazima tuhakikishe kuwa Israel haishiriki katika toleo lijalo la Eurovision,” na “ikiwa tutashindwa kufanya hivyo, Uhispania lazima isishiriki,” Ernest Urtasun ametangaza wakati wa mahojiano kwenye redio ya umma, msimamo ambao tayari umepitishwa na “Ireland, Slovenia, Iceland, na Uholanzi,” amebainisha.

“Mshikamano na watu wa Palestina”

Tayari mwezi Mei, Waziri Mkuu wa Kisoshalisti Pedro Sánchez alisema kuwa Israel inapaswa kutengwa kwenye Eurovision, maonyesho makubwa zaidi ya vipaji duniani, kutokana na “mshikamano” na “raia wa Palestina ambao wanakabiliwa na upuuzi wa vita na mashambulizi ya mabomu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *