.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Je, umeshawahi kukutana na vichwa vya habari vya namna hii?

“Mtindo mpya kwa wanawake utaharibu maadili ya jamii.”

“Afisa mmoja anashambulia baadhi ya jamii kwa maneno makali.”

“Mshawishi anamdhihaki mtu mlemavu kwenye video.”

Bila shaka jibu ni ndiyo na ndani ya dakika chache, sehemu ya maoni hujaa matusi, kejeli, wengine wakitaka kurekebisha, mashambulizi huku wengine wakitetea.

Watu wengi huchangia kutoa maoni na kuchapisha ujumbe licha ya wao kujua kuwa ujumbe huo umetiwa chumvi, muktadha wake sio sahihi, au hata unapotosha. Hata hivyo, wanachangia kwa sababu kupuuza hilo kunaonekana kuwa jambo lisilowezekana kwa wakati huo.

Ndani ya saa chache, ujumbe huo unasambaa kila mahali. Kwa nini? Kwa sababu tu ulifanikiwa katika jambo moja: kuchochea hasira.

Hili linaashiria jinsi majukwaa ya kijamii yalivyobadilika katika madhumuni yaliokusudiwa awali, namna ujumbe ulivyotengenezwa, kuboreshwa na kuwekwa katika majukwaa ya kijamii.

Pia, inaonyesha jinsi mjadala wa hasira ulivyogeuka na kuwa kichocheo cha majadiliano kwenye mitandao ya kijamii, namna ya kuvutia nadhari na wakati mwingine chombo cha kisiasa na usambazaji taarifa.

Lakini inamaana gani kusema kuwa majukwaa ya kijamii ni “kichocheo cha cha hasira”? Inatokeaje? Kwa nini imekuwa jambo linaloonekana kufanikiwa sana katika miaka ya hivi karibuni? Na inaonyesha nini kuhusu uhusiano wa watu na majukwaa ya kidijitali, mkondo wa kisiasa, na akili mnemba?

Hasira kama mkakati

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kamusi ya Oxford inafafanua “maudhui yanayochochea hasira” kama “maudhui ya kidijitali yanayotengenezwa kimakusudi ili kuchochea hasira au chuki kupitia uchochezi, kukatishwa tamaa au unyanyasaji, na kwa kawaida huchapishwa kwa lengo la kuvutia wachangiaji wa kidijitali.”

“Kusababisha hasira” ni sawa na aina zingine za kutaka kuvutia watu kuona ujumbe wako, kama vile vichwa vya habari vinavyovutia watumiaji wa majukwaa ya kijamii kutaka kujua zaidi huku lengo la aliyeweka ujumbe likiwa kupata watu wengi zaidi.

Hata hivyo, kinachotofautisha “uchochezi wa hasira” na mbinu zingine za kutafuta majadiliano kwenye mitandao ni kutegemea kwake kuchochea hisia za hasira, badala ya kuvutia nadhari au kuhimiza mwitikio chanya.

Ingawa “kuchochea hasira” au uchochezi wa makusudi haukutokana na kuibuka kwa mtandao, kilichojitokeza katika miongo miwili iliyopita ni mfumo unaowezesha “kuchochea hasira”, na kusababisha kuenea wake.

“Usababishaji hasira” kwa manufaa ya mtu hufanyaje kazi?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuchochea hasira” kunalenga uchochezi na kusababisha mwitikio wa haraka, si kubishana au kushawishi.

Maudhui yaliyoainishwa ndani ya mfumo huu hayajajikita kwa ulazima wa kubadilisha maoni ya wapokeaji, bali yanalenga kuyasukuma kuelekea mwitikio wa haraka na wenye ushawishi.

Hasira, tofauti na hisia zingine, huchochea mwitikio wa haraka: kujibu, kushirikisha, kuchapisha tena ujumbe, au hata kushambulia.

Kwa sababu hii, aina hii ya maudhui mara nyingi hutengenezwa kwa lugha kali, mtindo uliokithiri, au kwa kuwasilisha misimamo inayoonekana kuwa ya uchochezi au ya kupotosha kimakusudi.

Lengo si mjadala, bali ni kuvunja ukimya ambao unaweza kuambatana na hisia kali zaidi kama vile mashaka au mkanganyiko.

Hasira haiachi nafasi ya kutafakari; husababisha mwitikio wa haraka, wakati mwingine kabla ya kuthibitisha au kuzingatia muktadha.

Katika muktadha huu, majukwaa ya mitandao ya kijamii hayatofautishi kati ya majadiliano chanya na hasi. Yote mawili yanachukuliwa kuwa viashiria vya “maslahi” na huchangia kuongeza wanaofikia maudhui.

Hivyo, hasira hubadilishwa kutoka hisia hadi kichocheo muhimu cha taswira za kidijitali, iwe hasira hii inaelekezwa kwa kuunga mkono au kukataa jambo fulani.

Je, hasira inawezaje kubadilishwa kuwa thamani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mbinu za “udanganyifu” haziwezi kutambulika kwa kujitegemea na mtindo wa hivi karibuni zaidi ukiwa uwezo wa majukwaa ya kidijitali kuvutia na kudumisha watumiaji wa mitandao kwenye akaunti zao za kijamii kwa muda mrefu zaidi ndiyo kumekuwa chanzo kikuu cha thamani.

Kwa miaka kadhaa sasa, kuvutia umma kumekuwa zaidi ya hali ya kiakili tu; ni rasilimali adimu ambayo huwekezwa, kupimwa, na kubadilishwa kuwa data na kisha kuwa faida.

Katika sehemu yenye ushindani mkubwa wa kidijitali, hisia zinazoweza kuvutia nadhari haraka—miongoni mwao hasira—hupata faida dhahiri kwa sababu athari zake huonekana haraka.

Mtindo huu baadhi ya watafiti huuiita “cognitive capitalism,” ambapo uzalishaji hauzuiliwi tena na bidhaa au huduma, bali unasambaa hadi uwezo wa kiakili na kihisia wenyewe: kuvutia nadhari, hisia, na mwitikio. Hisia si tena masuala ya kibinafsi, bali zimekuwa sehemu ya mzunguko wa uzalishaji thamani ya kidijitali.

Hasira, hisia inayohamasishwa kwa urahisi zaidi kidijitali

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tukirudi nyuma miaka minane, kabla ya Kamusi ya Oxford kuwa na neno “inciting anger” yaani “kuchochea hasira” kama neno lake la mwaka wa 2025, Kamusi ya Cambridge ilichagua “populism” kama neno lake la mwaka wa 2017.

Katika muktadha huu, ni vigumu kutafsiri ongezeko la hasira kwenye majukwaa ya kidijitali katika miaka ya hivi karibuni peke yake bila kuangazia kuongezeka kwa mgawanyiko kati ya watu wa kawaida na wenye ushawishi.

Utafiti uliopewa jina la “”Populism Fuels Love and Anger: The Impact of Discourse Characteristics on User Interactions on Facebook,” uliochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Mawasiliano, unaonyesha kwamba hasira ndiyo hisia inayohamasishwa kwa urahisi zaidi kidijitali.

Maudhui ya kisiasa yanayotumia lugha ya kukera, kuwadhalilisha wanaojihusisha na siasa, au kuwalaumu “watu wa hali ya juu” au “wengine” hutoa majibu ya hasira kuliko mazungumzo ya uchambuzi au yasiyoegemea upande wowote.

Kwa kuwa majukwaa ya kidijitali hayatofautishi kati ya hasira na kuunga mkono, na yote mawili yanahesabiwa kama viashiria vya “maslahi,” kila mwitikio wa hasira huchangia kwa kiasi kikubwa kupanua uenezaji wa kushutumiwa.

Kwa hivyo, utafiti ulihitimisha kwamba watu wanaopenda umaarufu huogopa kutojali kuliko chuki. Hasira, iwe ya kuunga mkono au ya uadui, inawahakikishia uwepo na kujulikana.

Hasira bandia

Labda mabadiliko makubwa zaidi leo katika mikakati ya kuchochea hasira ni kwamba hasira hii imekuwa na uwezo wa kusababishwa moja kwa moja.

Katika utafiti uliopewa jina la “Generating AI to Incite Anger: Implications for Digital Harm,” published in the journal “New Media and Society,” mtafiti Rob Cover anasema kwamba akili mnemba imekuwa kichocheo huru cha maudhui yaliyoundwa kuchochea hasira ndani ya mfumo wa kidijitali wenyewe.

Hii haimaanishi tu kuongezeka maradufu kwa kiasi cha maudhui ya uchochezi, lakini pia uwezekano wa uchochezi wa hasira katika mfumo wa algoriti moja kwa moja, ambao huzidisha aina za Athari mbaya za majukwaa ya kidijitali na kusababisha mwelekeo mpya kwenye suala la nini kinachozalishwa, kinachotanuliwa, na kile kinachoachwa ili kutoweka katika majukwaa ya umma ya kidijitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *