Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kuwait imetangaza “kufungwa kwa muda kwa anga ya nchi ” hiyo kufuatia mashambulizi ya Iran, kama kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya anga ya Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hatua hii inafuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya taifa la Kuwait na hatari zinazoweza kutokea kwa usafiri wa anga wa kiraia katika eneo hilo,” mamlaka hiyo imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Jeshi la Kuwait limetangaza kuwa linailinda nchi hiyo dhidi ya shambulio la anga, baada ya Iran kudai kushambulia kambi mbili za kijeshi nchini humo.

“Mifumo ya ulinzi wa anga kwa sasa inashambulia malengo ya angani ya adui, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa za uendeshaji,” makao makuu ya jeshi la Kuwait limeandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *