Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amekiri “kutofautiana” na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye “amefanya makosa” katika vita vya Mashariki ya Kati, kulingana na dondoo zilizochapishwa siku ya Jumatano kutoka kwa mahojiano na CBS.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance  amebainisha kwamba Israel ni mshirika wa karibu sana wa Marekani, lakini “wakati mwingine maslahi yetu yanaendana kikamilifu na wakati mwingine yanatofautiana,” amesema katika dondoo iliyotolewa na kituo hicho cha habari kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X. Mahojiano hayo yamepangwa kurushwa hewani siku ya Jumapili.

“Nilichokiona na Waziri Mkuu ni kwamba anatetea kwa nguvu maslahi ya nchi yake. Wakati mwingine hiyo ina maana kwamba tunakubaliana na hicho anachoongea, na wakati mwingine hapana,” ameongeza.

Uhusiano kati ya Donald Trump na kiongozi wa Israel umekuw mgumu katika wiki za hivi karibuni, huku rais wa Marekani akienda mbali zaidi na kumwambia Benjamin Netanyahu kwamba ni “mwendawazimu kabisa” wakati wa mazungumzo ya simu ya hivi karibuni, kulingana na tovuti ya Axios.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *