
Iran imeiomba Washington kusitisha mashambulizi katika eneo lake, mwandishi wa habari wa Fox News amebainisha, akimnukuuRais wa Marekani Donald Trump.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maafisa wakuu wa Iran wamemwomba Donald Trump kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran, kulingana na mwandishi wa habari wa Fox News ambaye anasema alizungumza na rais wa Marekani kwa simu.
“Rais Trump ameniambia kwamba Iran ilimpigia simu usiku wa leo,” amesema mwandishi wa habari Trey Yingst. “Ameniambia kwamba Maafisa wakuu wa Iran walimwomba kusitisha mashambulizi ya angani,” ameiambia Fox News. Rais wa Marekani pia alimhakikishia kwamba “mashambulizi yatasitishwa hivi karibuni,” mwandishi huyo almesema.
Tehran imekanusha mara moja madai hayo, kulingana na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), jeshi la kiitikadi la Iran, katika taarifa. “Madai ya Trump kwamba maafisa wa Iran waliwasiliana naye yanakanushwa vikali na ni kisingizio tu cha kuepuka vita,” IRGC imesema.