#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Mhe. Deus Sangu, amesisitiza umuhimu wa uwepo wa mabaraza ya wafanyakazi, katika Taasisi za Umma na Binafsi, huku akisema kuwa ni chombo muhimu cha kushauri na kuimarisha ukuaji wa taasisi kiuchumi.
Waziri Sangu amebainisha haya wakati wa uzinduzi wa Baraza la Tatu la Wafanyakazi la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), na kwamba mabaraza ya wafanyakazi yanatambuliwa kisheria na yanapaswa kutumika kutoa ushauri wenye tija kwa manufaa ya taasisi na taifa kwa ujumla.
Amesema bado kuna changamoto katika sekta binafsi, ambapo baadhi ya waajiri hawaruhusu uwepo wa vyama vya wafanyakazi wala kuundwa kwa mabaraza, wakidhani kwamba vyama hivyo vinavizuia kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Waziri Sangu ameonya kuwa kama mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya vyama vya wafanyakazi nchini, hatasita kuchukua hatua dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria, akisisitiza kuwa ushiriki wa wafanyakazi kupitia vyama vyao husaidia kuongeza uzalishaji, jambo linaloongeza mapato ya Serikali kupitia kodi.
Kwa upande wake, Silvester Issaya, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda na Biashara Tanzania (TUICO), amesema wafanyakazi wa sekta zote za umma na binafsi ni nguzo muhimu katika kuboresha taasisi, na kusisitiza kuwa vyama vya wafanyakazi vitaendelea kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi yanazingatiwa kisheria.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa PSSSF na pia Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Fortunatus Magambo, wamesema uwepo wa baraza la wafanyakazi umeleta mafanikio makubwa, kwani ushauri unaotolewa umechangia kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radiooneta