#HABARI: Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Februari 05, 2025 katika Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, yakihusisha wanachama wa CCM, viongozi wa chama na Serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katika kuadhimisha miaka hiyo 49 tangu kuanzishwa kwake, Chama Cha Mapinduzi kimepanga kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuleta mchango chanya kwa jamii, miongoni mwa shughuli hizo ni upandaji wa miti zaidi ya Elfu kumi kama sehemu ya juhudi za utunzaji wa mazingira, pamoja na uchangiaji wa damu katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Kigoma, ili kusaidia kuokoa maisha ya wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radiooneta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *