
Taasisi ya Jacob Zuma imetoa taarifa kali baada ya jina la rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kutajwa katika hati mpya za wazi mahakama zenye mfungamana na Jeffrey Epstein, mfadhili na mhusika wa kashfa za ngono aliyefia jela huko Marekani.
Barua pepe ya mwaka 2010 inadaiwa kumhusisha mshirika wa Epstein kwa jina la Mark Lloyd, akijadili suala la kuandaa chakula cha jioni katika hoteli ya London kwa ajili ya rais wa wakati huo wa Afrika, Kusini Jacob Zuma.
Ujumbe huo wa barua pepe aidha ulipendekeza kumwalika mwanamke kwa jina la Vera kwa ajili ya kupendezesha zaidi karamu hiyo ya chakula cha jioni. Barua pepe hiyyo ilimtaja Zuma kama “shakhsia wa kuvutia” katika mwaliko huo.
Taaisi ya Jacob Zuma imekanusha kuhusika na mhalifu huyo. Msemaji wa taasisi hiyo, Mzwandele Manyi, amekosoa ripoti hizo na kuzitaja kuwa hatua isyo ya kimaadili yenye lengo la kuchafua taswira ya Zuma.
Msemaji wa Taasisi ya Jacob Zuma amekanusha simulizi hiyo aliyoitaja kuwa ya kukisia iliyojificha chini ya mwavuli wa uandishi wa habari za uchunguzi na kusema mjadala huo umefungwa.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, nyaraka zinazohusiana na Jeffrey Epstein, bepari na bilionea aliyepatikana na hatia ya biashara ya ngono ya watoto, zimeanika peupe uhusiano wa siri aliokuwa nao na watu mashuhuri na vilevile shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad.
Mlanguzi huyo wa ngono pia alikuwa na mawasiliano na baadhi ya watu mashuhuri wa Marekani, wakiwemo Kevin Spacey na Chris Tucker, na pia amemshauri Elon Musk kuhusu mambo tofauti.
Epstein aliunda mduara wa watu mashuhuri na kuwawezesha kutumia kingono idadi kubwa ya wanawake na watoto, ambapo alishirikiana na wasaidizi wake kuwanyanyasa kingono.