VIWANJANI: “Mimi bado nawapa nafasi…”
Mchambuzi wa soka Philip Nkini amesema bado ana imani na Azam FC kuendelea hatua ya robo fainali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) endapo watashinda michezo yao iliyobaki.
Nkini amesema ushindi ndio njia pekee itakayomvusha Azam kucheza hatua inayofuata bila kufikiria matokeo ya wapinzani wake.
Azam FC itamenyana na AS Maniema Februari 7, katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports3HD
Imeandikwa na Katherini Shirima
Mhariri: @allymufti_tz