LUDEWA WALIA KUKATIKA KWA UMEME MARA KWA MARA.
Wakazi wa wilaya ya Ludewa wameiomba serikali kupitia shirika la Umeme TANESCO, kushughulikia maramoja changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali inayowapa hasara na kukwamisha shughuli za kiuchumi.
Tatizo la kukatika kwa umeme ludewa limetajwa kuwa kero kubwa kwa wakazi wa Kata ya Ruhuhu mwambao mwa ziwa Nyasa, wakazi wa Ludewa mjini na Kata ya Mlangali ambapo baadhi yao akiwemo Peter Mahundi na Hanifa Luoga, wamesema tatizo hilo ni la muda mrefu na bado halijapata ufumbuzi huku muda mwingine wanalazimika kushinda siku nzima bila umeme hali inayokwamisha shughuli za kimaendeleo wilayani humo.
Mbele ya mbunge wao Joseph kamonga wamemtaka aisisitize serikali kutatua chanagamoto hiyo maramoja ili shughuli za uzalishaji na ujasiriamali ziweze kufanyika kwa uhakika kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Kukosekana kwa nishati hiyo zaidi ya mara nne hadi tano kwa siku na wakati mwingine kukosekana kabisa kunatajwa kudidimiza shughuli za viwanda na ujasirimali ambao wakati wote wanategemea nishati ya umeme kuendesha shughuli zao.
Kamonga ameahidi kuibeba changamoto hiyo na kuiwasilisha serikalini maramoja ili kupata ufumbuzi wa nini hasa chanzo cha kukatika kwa umeme mara kwa mara katika wilaya ya Ludewa.
#HabariStartv
#RFAOnline
@dkhan1410.