
Dar es Salaam. Katika hatua muhimu ya kukuza ujumuishaji wa huduma za kidijitali nchini, Yas imeungana na Xiaomi, kuzindua toleo jipya aina ya Redmi Note 15 Series hapa nchini.
Redmi Note 15 Series ni toleo la kisasa la simu yenye uwezo mkubwa inayouzwa kwa bei rafiki, na simu hii ni moja ya zana za kidijitali yenye umuhimu mkubwa kwa masomo, biashara, na mawasiliano ya kila siku.
Redmi inakuja na matoleo mbalimbali kwa bei tofauti kama ifuatavyo:-
● Redmi Note 15 (6+128GB) – TZS 575,000
● Redmi Note 15 (8+256GB) – TZS 660,000
● Redmi Note 15 Pro (256GB, 5G) – TZS 850,000
● Redmi Note 15 Pro+ (256GB, 5G) – TZS 1,150,000
Kupitia ushirikiano huu, Yas inaendelea kuimarisha nafasi yake sokoni kama mshirika sahihi wa kidijitali anayewawezesha Watanzania kufanikisha maisha yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Ikunda Ngowi, Meneja wa Vijana na Wateja Maalum Yas, alisisitiza kuhusu mchango mkubwa unaoletwa kupitia ushirikiano huu kwa watumiaji wa Yas.
“Vijana na wafanyakazi wa kipato cha kati ndio wanaochangia ukuaji mkubwa wa kidijitali Tanzania, lakini kupata vifaa vinavyoweza kuwasaidia kujifunza zaidi, ubunifu na biashara bado ni changamoto. Redmi Note 15 Series inabadilisha hali hiyo. Hii ni simu yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi mbalimbali na kuleta matokeo chanya kwa watanzania. Simu hii inapounganishwa na huduma za Yas, inakua ni zaidi ya simu na kurahisisha maisha ya watengeneza maudhui, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wakulima katika maeneo ya pembezoni”.
Kwa upande wake, Eric Mkomoye, Meneja wa Masoko wa Xiaomi Tanzania, alisema, “Dhamira ya Xiaomi ni kuendelea kuwaletea watanzania teknolojia bora. Redmi Note 15 Series ni toleo linalokuja na mambo mengi mazuri kuanzia utendaji, muundo, na bei rafiki, yote yakiifanya simu hii iwe chaguo bora kwa Watanzania wanaohitaji simu za kuaminika kwa bei rafiki. Ushirikiano wetu na Yas unatuwezesha kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuhakikisha wafanyabiashara, wanafunzi, wajasiriamali na watumiaji wa kawaida wanaunganishwa kufanya miamala, na kukua kidijitali.”
Kadiri Tanzania inavyoendelea kukua kidigitali, ushirikiano wa Yas na Xiaomi unahakikisha huduma za kidigitali si kwa ajili ya watanzania wachache tu bali kwa watanzania wote.
Redmi Note 15 Series sasa inapatikana kwenye maduka ya Yas na wauzaji wa Xiaomi waliothibitishwa kote nchini.