India imeongeza kodi kwenye sigara na bidhaa za tumbaku, ikiongeza kiwango cha msingi cha kodi kutoka asilimia 28 hadi asilimia 40 kuanzia mwezi huu.

Wazalishaji wa tumbaku na watu wengine katika sekta hiyo wana wasiwasi kwamba hii itasababisha kupotea kwa ajira, kuongezeka kwa magendo au biashara zingine haramu ikiwa ni pamoja na bidhaa bandia.

Mwaka jana, serikali ilipunguza kodi ili kuchochea matumizi ya ndani kufuatia bidhaa za India kutozwa ushuru wa forodha wa juu na Marekani. Ongezeko la kodi ya tumbaku lilikusudiwa kufidia hasara kutokana na kodi zingine.

Hatua hiyo inaweza kuongeza bei ya pakiti ya sigara kwa rupia 55, au takriban senti 60, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi.

Mwanamume mmoja anayemiliki duka la sigara alisema kwamba athari ya ongezeko la kodi itakuwa kubwa. “Mauzo yanaweza kushuka kwa asilimia 100 ndani ya miezi miwili hadi mitatu,” aliongeza.

Inasemekana kuna takriban wavutaji sigara milioni 250 nchini India.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *