
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Brazil imetangaza siku ya Jumatatu, Septemba 22, kufunguliwa mashitaka kwa mmoja wa watoto wa kiume wa rais wa zamani Jair Bolsonaro kwa kuzuia kesi ya baba yake, aliyepatikana na hatia ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi, akimtuhumu kwa kushawishi mamlaka ya Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mbunge Eduardo Bolsonaro, anayeisi uhamishoni nchini Marekani anashukiwa “kutishia mamlaka ya mahakama na mamlaka zingine” kwa kudai kwamba atapata vikwazo dhidi ya taasisi hizi “kutoka kwa mamlaka ya Marekani,” kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka.
Hayo yanajiri wakati Marekani ilitangaza vikwazo siku ya Jumatatu dhidi ya mke wa Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil Alexandre de Moraes, ambaye aliongoza kesi iliyopelekea rais wa zamani Jair Bolsonaro kutiwa hatiani, kesi ambayo ilikuwa katikati ya mgogoro kati ya nchi hizo mbili.
Donald Trump na serikali yake wamekuwa wakitoa shinikizo kwa mamlaka ya mahakama ya Brazil kwa miezi kadhaa, wakiwatuhumu kwa kumfungulia mashtaka isivyo haki aliyekuwa rais wa mrengo mkali wa kulia wa Brazil Jair Bolsonaro, mshirika wa rais wa Marekani.
Jaji Alexandre de Moraes, mlengwa mkuu wa mamlaka ya Marekani, amekuwa akiwekewa vikwazo vya kiuchumi tangu mwisho wa mwezi wa Julai, huku Washington ikimtuhumu kwa “kupanga kesi isiyo ya haki” dhidi ya Jair Bolsonaro.
Elon Musk, ambaye yuko karibu na Donald Trump licha ya kuachana kwao, alimlinganisha jaji huyo na Voldemort, mhalifu katika sakata ya Harry Potter.
Vikwazo hivyo vipya vilivyotangazwa siku ya Jumatatu na Wizara ay Fedha ya Marekani vinamlenga mke wa jaji huyo, Viviane Barci de Moraes, pamoja na kampuni inayohusishwa na familia hiyo.
Vikwazo hivyo vinasababisha kuzuiwa kwa mali zao zote zinazoshikiliwa nchini Marekani na kupiga marufuku raia wa Marekani au makampuni yanayofanya biashara nao, chini ya adhabu ya kufunguliwa mashitaka.