
Makabiliano kati ya magenge hasimu katika gereza moja kusini-magharibi mwa Ecuador yamesababisha vifo vya watu 14, wakiwemo wafungwa 13 na mlinzi mmoja, polisi katika nchi hiyo ya Amerika Kusini inayokumbwa na ghasia imetangaza Jumatatu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya kuingia katika gereza la Machala, polisi wamegundua miili ya “watu 14 waliofariki,” afisa wa polisi aliyejifunika uso amekiambia kituo cha habari cha Ecuavisa. Pia amesema watu 14 walijeruhiwa na “wafungwa wengine” ambao walitoroka, 13 kati yao wamepatikana baadaye.
Polisi wameripoti kuchukua udhibiti wa gereza hilo, ambalo lina uwezo wa kupokea takriban wafungwa 600 lakini lina wafungwa kwa sasa mara mbili zaidi. Milio ya risasi ilisikika mwendo wa saa 8:00 usiku kwa saa za huko, ikiwatahadharisha askari magereza na maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda majengo hayo. Mapigano kati ya makundi hasimu yalichukua takriban dakika 40, na wafungwa walitumia bunduki, “mabomu, na maguruneti,” kulingana na Kamanda Calle.
Kituo cha kuanzia usafirishaji kwa 70% ya kokeini ulimwenguni
Nchi hii yenye watu milioni 18, iliyo kati ya wauzaji wakubwa wa kokeini duniani, Colombia na Peru, inakabiliwa na wimbi la vurugu ambalo halijawahi kushuhudiwa kutokana na makabiliano kati ya magenge ya wahalifu wanaohusishwa na magenge ya Mexico na Colombia. Imekuwa kituo cha kuhifadhi dawa za kulevya na kituo cha kuanzia usafirishaji kwa 70% ya kokeini ulimwenguni, karibu nusu ambayo inaelekezwa kwa soko la Marekani, kulingana na data rasmi.
Magereza ya Ecuador yamekuwa vituo vya operesheni za makundi ya wafanyabiashara haramu wa dawa za kulevya kwa miaka kadhaa. Mara kwa mara huwa eneo la mauaji, hali ambayo imesababisha vifo vya wafungwa wasiopungua 500 tangu mwaka 2021.