Inadaiwa kuwa ukuaji wa kizazi cha sasa na cha zamani unaonyesha tofauti kubwa. Kizazi kilichozaliwa kuanzia mwaka 2000 kinaonekana kuzeeka kwa haraka kimuonekano, yaani umri wao halionekani kulingana na ukubwa wa mwili wao.
Afisa na mtafiti wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula (TFNC), Abela Twinomujini ameeleza kuwa moja ya sababu zinazochangia hali hii ni mwenendo wa vyakula wanavyokula, ikiwemo lishe isiyofaa na matumizi ya vyakula vilivyochakatwa sana.
#AzamTVUpdates
✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi