
Waziri Mkuu wa Misri Mustafa Madbouly ametangaza siku ya Jumatatu, Septemba 22, kuwa nchi yake itakuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu ujenzi wa Gaza mara tu usitishaji wa mapigano utakapokamilika katika ardhi iliyoharibiwa ya Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Misri itakuwa mwenyeji, punde tu usitishaji vita utakapofikiwa, mkutano wa kimataifa kuhusu ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza ili kukusanya fedha zinazohitajika kwa ajili ya mpango wa ujenzi kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu,” amesema katika mkutano wa suluhisho la mataifa mawili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Wakati huo huo, akizungumza siku ya Jumatatu mwanzoni mwa mkutano huo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametangaza kuwa nchi yake sasa inalitambua rasmi taifa huru la Palestina.
Macron amesema lazima wafungue njia kwa ajili ya amani, na kuhakikisha kuna uwezekano wa suluhisho la mataifa mawili, ambapo Israel na Palestina zitaishi pamoja kwa amani na usalama.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan Al Saud, ameupongeza uamuzi huo wa Rais Macron akisema ni wa kihistoria, na kuzitaka nchi nyingine kuchukua hatua kama hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema taifa huru la Palestina ni “haki na sio zawadi.”