Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeeleza kuwa watoto wa Kipalestinan wasiopungua 37wameuawa katika mashambuliiz ya Israel huko Gaza tangu kuanza mwaka huu wa 2026.

Taarifa ya UNICEF imeeleza kuwa, Edouard Beigbeder Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF katika Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amesema kuwa “hali bado ni “hatari na mbaya sana” kwa watoto wengi huko Gaza licha ya usitishaji vita unaolegalega wa mwezi Oktoba mwaka jana katika eneo hilo llililo chini ya mzingiro.

Ameongeza kuwa watoto wanaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya anga, huku sekta ya afya, maji, na mifumo ya elimu ikiwa imeathirika pia. 

Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF katika Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika pia ametilia mkazo kuhusu haja ya kuendelea kutekelezwa usitisaji vita Gaza ili kuhitimisha mateso na masaibu kwa watoto wa ukanda huo.  

Mnamo Januari mwaka huu, James Elder Msemaji wa Shirika la UNICEF  alisema kuwa zaidi ya watoto 100 wa Kipalestina, wakiwemo wavulana 60 na wasichana 40 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kutekeleza mapatano ya kusitisha vita mwezi Oktoba mwaka jana.  

Elder amesisitiza kuwa idadi hi ni ya chini kabisa, kwa sababu idadi halisi ya vifo miongoni mwa watoto wa Kipalestina inatarajiwa kuwa kubwa zaidi. Ameashiria pia athari mbaya za mashambulizi ya kikatili ya Israel kwa sekta ya huko Gaza, ambapo takriban asilimia 90 ya shule zimeharibiwa au kubomoka kikamilifu, na kupelekea zaidi ya watoto 700,000 wa KIpalestina kusalia bila  elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *