Shule ya Kimataifa ya Arusha Meru iliyopo jijini Arusha imefungua rasmi sehemu maalum ya maktaba ijulikanayo kama India Book Corner, mpango unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kielimu na kitamaduni kati ya Tanzania na India.

Hafla hiyo imewakutanisha uongozi wa shule, walimu, wanafunzi pamoja na wawakilishi wa ubalozi wa India nchini, ikiwa ni hatua ya kuongeza fursa za wanafunzi kujifunza kuhusu jamii na maarifa ya kimataifa kupitia vitabu.

India Book Corner inajumuisha vitabu vinavyoangazia historia, utamaduni, sayansi na falsafa ya India, huku wanafunzi wakipata nafasi ya kusoma kazi za viongozi mashuhuri akiwemo Mahatma Gandhi na A. P. J. Abdul Kalam, pamoja na simulizi zinazoakisi maisha ya kisasa ya nchini humo.

✍ Ramadhan Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *