Yanga itaanza kutetea taji lake la Shirikisho la CRDB kwa kukabiliana na Cosmopolitan wiki ijayo kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa hatua ya 64 bora ya mashindano hayo ambayo bingwa wake anapata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika droo ya hatua hiyo iliyofanyika Dar es Salaam leo, mabingwa mara tatu wa mashindano hayo, Simba wamepangwa kukutana na Greenland FC ya Kagera.

Azam FC ambayo ilitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2019 nayo itaanzia nyumbani kwa kuikaribisha Endument ya Kilimanjaro.

Wana fainali wa msimu uliopita, Singida Black Stars nao wataanzia nyumbani kwa kucheza na Copco ya Mwanza wakati huo KMC ikipangwa kucheza na Bandari Tanzania.

Kutakuwa na mchezo wa watani wa jadi wa mkoa wa Tabora ambao utazikutanisha TRA United na Rhino Rangers na mwingine wa mkoa wa Dar es Salaam baina ya JKT Tanzania na Pan African.

Mabingwa wa zamani wa mashindano hayo, Mtibwa Sugar watacheza na IAA na Coastal Union wataikaribisha Nyumbu FC.

Ofisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema kuwa mechi hizo zitachezwa wiki ijayo.

“Kuna baadhi ya viwanja vinatumika na timu zaidi ya moja kwa hiyo lazima zipeane nafasi lakini hatua ya 64 bora itachezwa kuanzia tarehe 17 Februari hadi tarehe 19 Februari,” amesema Kizuguto.

Mechi za 64 Bora Kombe la Shirikisho la CRDB

Mbeya Kwanza vs FGA Talent

Kagera Sugar vs Mighty Elephant

Geita Gold vs Kajuna

Kengold vs Magereza FC

B19FC vs Dhujau

Mbuni vs The Green FC

Transit Camp vs Chama la Wana

Barberian vs Kijiwe Nongwa

Songea United vs Vijana FC

Gunners FC vs Airport FC

Bigman vs Nyika

TMA vs Newala FC

Polisi Tanzania vs THB

Hausung vs West Singers

Stand United vs Mabao

African Sports vs Kilimo FC

Tanzania Prisons vs Moro Kids

Mbeya City vs Biashara United

Coastal Union vs Nyumbu FC

TRA United vs Rhino Rangers

Simba vs Greenland FC

JKT Tanzania vs Pan African

Mtibwa Sugar vs IAA

Fountain Gate vs Mapinduzi

Namungo FC vs Magnet FC

Pamba Jiji vs Alliance

Dodoma Jiji vs Kilimanjaro Wonders

Yanga vs Cosmopolitan

Azam FC vs Endument FC

Singida Black Stars vs Copco

KMC vs Bandari Tanzania

Mashujaa vs Nkim FC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *