#HABARI: Mchungaji Rose Masesa, dada mkubwa wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuangalia upya kesi ya uhaini inayomkabili mdogo wake.

Akizungumza leo Februari 09, 2026, jijini Dar es Salaam, Mchungaji Rose amebainisha kuwa familia ilishangazwa na shtaka hilo kwani Lissu amekuwa akipigania utawala wa sheria na ulinzi wa haki za binadamu.

Mchungaji Rose ametoa rai kwa Serikali kutafakari mara mbili kuhusu kesi hiyo, akidai kuwa uwepo wake unaendelea kuleta mgawanyiko katika jamii.

Amesisitiza kuwa Tundu Lissu ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani mwenye wafuasi wengi, hivyo kuendelea kwa kesi hiyo kunaweza kutoleta tija katika ujenzi wa umoja wa kitaifa.

Maombi hayo yametolewa kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambapo Mchungaji Rose ameweka wazi kipaumbele cha Lissu mara zote kimekuwa ni kupigania taifa.

Familia inaamini kuwa kurekebishwa kwa mwenendo wa kesi hiyo kutaonyesha dhamira ya dhati ya serikali katika kukuza demokrasia na haki nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *