Wataalamu wa afya wameonya kuwa si salama kutumia jiko la mkaa ndani ya nyumba kutokana na hatari kubwa ya kiafya inayoweza kusababisha, ikiwemo vifo, hasa kwa watoto.
Onyo hilo linatolewa kufuatia kuendelea kuripotiwa kwa matukio ya watoto kufariki kutokana na kuvuta moshi wa jiko la mkaa wakiwa ndani ya nyumba.
Tukio la hivi karibuni limetokea mkoani Manyara, ambapo mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane amefariki dunia, huku watu wengine wawili wakinusurika kifo baada ya jiko la mkaa lililowashwa kuachwa ndani ya chumba walichokuwa wakiishi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)