Afrika Kusini imetangaza uamuzi mzito wa kisera na kiusalama, kuanza kuwaondoa wanajeshi wake waliokuwa wakihudumu chini ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Pretoria, Rais Cyril Ramaphosa alimuarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwamba uamuzi huo umetokana na haja ya kuyafanyia mageuzi vikosi vya ulinzi vya Afrika Kusini.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *