Akiendelea na mashauriano yake ya kikanda, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Muscat mapema leo akiongoza ujumbe wa ngazi za juu na kufanya mazungumzo na Mfalme Haitham bin Tariq katika mkutano ulioendelea kwa karibu saa tatu.

Mkutano huo umefanyika katika mazingira chanya na yenye kujenga, na umejadilii matukio ya hivi karibuni ya kikanda na kimataifa, pamoja na njia za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Baada ya mkutano wake na Sultan Haitham bin Tariq, Dakta Ali Larijani pia amekutana mara moja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaid.

Itakumbukwa kwamba kwa ssa Oman ni mwenyeji wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran. Mazungumzo hayo yalianza Ijumaa, Februari 7.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye aliongoza timu ya mazungumzo ya Iran katika duru ya kwanza ya mazungumzo hayo, alisema mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja na Marekani huko Muscat Oman yamekuwa na mwanzo mzuri, na kwamba hatua za baadaye zinasubiri mashauriano katika miji mikuu.

Alisisitiza kwamba Iran ilielezea waziwazi mitazamo yake, wasiwasi na haki na maslahi ya watu wa Iran katika mazingira chanya sana.

Ajenda kuu ya mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja ni faili la la nyuklia la Iran na kuondolewa vikwazo taifa hili vilivyowekwa na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *