#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Mohamed Rashid Mumpa, mmiliki wa gari la abiria aina ya Hiace yenye namba T 234 BUM, kufuatia tukio la kutelekezwa kwa gari hilo baada ya kuwagonga na kuwajeruhi watu wawili, akiwemo askari wa usalama barabarani.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la mzunguko wa barabara ya Kenyatta jijini Mwanza wakati askari huyo akiwa kazini, huku jeshi hilo likiendelea na msako mkali wa kumtafuta dereva wa gari hilo aliyetoroka mara baada ya kusababisha ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, amesisitiza kuwa wataendelea kuchukua hatua kali dhidi ya madereva na wamiliki wa vyombo vya moto wanaoshindwa kuheshimu sheria za usalama barabarani.

Wakati askari na mjeruhiwa mwingine wakiendelea kupata matibabu, baadhi ya wakazi wa jijini Mwanza wameilaani ajali hiyo na kuliomba jeshi la polisi kuongeza udhibiti ili kuzuia ajali zisizo za lazima zinazohatarisha maisha ya watu na watendaji wa Serikali.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *