
Mgombea wa chama cha Republican katika nafasi ya gavana wa Florida, James Fishbach, amezua mzozo wa kisiasa baada ya shambulio lake la moja kwa moja dhidi ya Ukuta wa Magharibi (Wailing Wall) na ahadi yake ya kukata uhusiano wote wa kiuchumi na Israel kama atashinda kiti hicho.
Gazeti la Hayom la Israel limeripoti kuwa, Fishbach ametoa matamshi hayo katika hotuba yake kwenye Chuo Kikuu cha Central Florida, ambapo alitangaza kuwa anapinga vikali kutembelea Israel iwapo atachaguliwa, na kwamba anapendelea kuzingatia nchi zingine kwa ajili ya kutengeneza ajira katika jimbo lake badala ya dola la Israel.
“Sitatembelea Israel… Napendelea kusafiri kwenda Brazil na nchi nyingine badala ya kutembelea dola ili kubusu ukuta wa kijinga,” amesema Fishback katika ujumbe wake kwenye jukwaa la X, akimaanisha Ukuta wa Magharibi, ambao Waisraeli wanauita “Ukuta wa Kulia (Wailing Wall).
James Fishbach amesema kwamba atafanya juhudi za kujitenga na Israel, akielezea kwamba hii itajumuisha kuondoa uwekezaji wote wa serikali ya jimbo la Florida kwenye dhamana za Israel, siku yake ya kwanza baada ya kuchaguuliwa, na kusisitiza kwamba suala hilo litarejesha Florida dola milioni 385 ambazo ilikuwa ikitumia huko Israel.
Fishback, mkandarasi wa zamani, aliingia katika kinyang’anyiro cha ugavana wa Florida mwaka wa 2025, akijaribu kuwa mbadala wa uongozi wa chama cha Republican chini ya uongozi wa jadi wa jimbo hilo, unaoongozwa na Mbunge Byron Donalds, anayeungwa mkono na Rais Donald Trump.
Chuki na misimamo inayoipinga Israel imeshika kasi zaidi nchini Marekani na katika nchi za Magharibi kwa ujumla kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Isarel kwa msaada wa Magharibi huko Palestina. Karibu Wapalestina elfu 72 wameuawa na Israel kwa silaha na misaada ya nchi za Magharibi hususan Marekani.