#HABARI: Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, amewahimiza wafanyabiashara nchini kuitumia Bandari ya Mtwara kutokana na fursa kubwa iliyonayo ikilinganishwa na Bandari ya Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara ya kukagua utendaji wa bandari hiyo na ujenzi wa Bandari ya Mizigo Michafu katika Kisiwa cha Mgao, Mhe. Kihenzile ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kuongeza kasi ya kutafuta masoko ya uhakika ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya miundombinu hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara ameisistiza serikali kuendelea kuibua masoko mapya yatakayohakikisha Bandari ya Mtwara inabaki na mzunguko mkubwa wa biashara hata baada ya mizigo michafu kuhamishiwa Kisiwa Mgao.
Wakati huohuo, Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara ameeleza kuwa bandari hiyo imeendelea kupata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma, jambo linalotoa imani kwa watumiaji na wadau wa usafirishaji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)