#HABARI: Vilio vya furaha vimetawala katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Singida huku baadhi ya wananchi wakipoteza fahamu kwa hisia, kufuatia kutatuliwa kwa kero sugu za dhuluma ya nyumba, viwanja na madai ya muda mrefu.
Mafanikio hayo yametokana na utekelezaji wa “Kikosi Kazi Samia” cha kutatua kero za wananchi, ambacho chini ya Mwenyekiti Wakili Said Omary, kimefanikiwa kutatua zaidi ya kero 900 zilizokuwa zikiwatesa wakazi wa Singida kwa miaka mingi.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali ya awamu ya sita huku akitoa maelekezo ya kudhibiti migogoro ya ardhi, mirathi na dhuluma inayojitokeza mara kwa mara.
Aidha, amewashauri wananchi kufuata sheria na taratibu ili kuepuka migogoro hiyo, akibainisha kuwa kila Alhamisi imetengwa rasmi kwa ajili ya kusikiliza na kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wilayani humo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)