OFISI ya msajili wa vyama vya siasa imevitaka vyama vya siasa nchini kuzingatia masuala ya jinsia kwa kuhakikisha vinatoa fursa na nafasi ya wanawake kushiririki kwenye masuala mbalimbali na kufanya siasa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza ametoa rai hiyo kwenye kikao kazi kwa wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania mjini Morogoro.
“Demokrasia inapaswa kuwa shirikishi kwa wanaume na wanawake kuwe na uwiano sawa,” amesema Nyahoza.

Nyahoza amesema kwa sasa kumekuwa na idadi kubwa ya wanawake ambao wanashiriki katika siasa na hata katika Baraza la Vyama vya Siasa .
Hivyo amesema kikao kazi hicho kimelenga kuwakumbusha viongozi wa vyama vya saisa kuhusu masharti yaliyopo katika sheria zinazosimamiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini .
Nyahoza amesema shughuli za vyama vya siasa vyote vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na sheria hizo ni ya vyama vya siasa, sheria ya gharama za uchaguzi ,katiba ya vyama vya siasa na kanuni za vyama vya siasa.
Amesema ili kuleta ufanisi katika uendeshajiwa vyama vya siasa kuwa wakizingatia sheria hizo ,ni kwamba masuala yao ya kiutendaji yanaweze kuwa mazuri na hivyo kuepuka kuwepo kwa migogoro ndani ya vyama vya siasa.

Nyahoza amesema kwa kuzingatia sheria hizo zinawasaidia pia kuwa na sera nzuri ambazo hazipingani na sheria nyingine za nchi ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Saum Rashid amepongeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwakutanishaa viongozi wa vyama vyote vya siasa ili kuwajengea uelewa wa kujifahamu sheria hizo na namna ya kusizimamia wakati wa majukumu yao .
Saum ambaye alikuwa mgombea urais kupitia chama hicho uchanguzi wa 2025 anasema kuwa endapo viongozi wa vyama vya siasa wanakuwa na uelewa wa sheria hizo zitawasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu, kuweka amani na utulifu katika nchi.
Pia amesema kuwashirikisha viongozi wa jumuiya za wanawake wa vyama vya siasa ambao si wajumbe kisheria na kupata mafunzo ni hatua muhimu ya kujenga demokraia pana na uelewa wa pamoja katika masuala ua sheria hizo.
Amesema wanawake wanaouwezo wanapopata fursa akitolea mfano wake alipata fursa ndani ya siasa kwa kuaminiwa na chama chake kuogombea urais ambayo ni nafasi kubwa.

“ Vipo baadhi ya vyama imewapa fursa kubwa wakiwa ni viongozi wazuri na hata wale waliokuwa wameshiriki kampeni walipokelewa vyema katika mikutano,” amesema Saum.
“ …Uongozi ni hekima, burasa na maarifa ndiyo njia kuu ya mwanamke hivyo vyote anavyo na kuendelea kuwaamini wanawake kwenye uongozi ni uelekezo muhimu katika kujenga taswira ya demokrasi,” amesisitiza.
Katika kikao kazi hicho mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo ya marekebisho yaliyofanyika mwaka 2024 katika Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria za Gharama za Uchaguzi na nyingine ya marekebisho yaliyofanyika mwaka 2025 katika kanuni.