ENGLAND: Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz, amepata jeraha la misuli na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kingine.
Mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani atakosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brentford utakaochezwa leo na huenda pia akakosa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili.
Arsenal wanatarajiwa kukutana na wapinzani wao wa jadi wa Kaskazini mwa London, Tottenham, Februari 22 na Havertz pia yuko hatarini kuukosa mchezo huo.
Pia kuna hatihati kuzikosa hadi mechi nne, huku Gunners pia wakitarajiwa kucheza dhidi ya Wolves wiki ijayo.
SOMA ZAIDI:
Havertz amekuwa akisumbuliwa na majeraha alirejea hivi karibuni kutoka kwenye tatizo la goti alilopata katika mechi ya ufunguzi wa msimu, ambalo lilimuweka nje kwa takribani miezi mitano.
Kabla ya jeraha hilo, Havertz alipata tatizo la msuli wa paja (hamstring) wakati wa mazoezi Dubai Februari 2025 na alifanyiwa upasuaji, hali iliyomfanya akose mechi za mwishoni mwa msimu uliopita.
Jeraha lake la sasa ni pigo kwa kocha Mikel Arteta, ambaye pia hana huduma ya kiungo Mikel Merino aliyefanyiwa upasuaji wa tatizo la mguu.
