[ad_1]

Kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amedai kuwa haoni kinachoendelea katika eneo hilo kuwa ni mauaji ya kimbari.

Macron ameendelea kudai kwamba hii sio taarifa ya kisiasa na kwamba ni majaji au wanahistoria pekee ndio wanaweza kutambua tukio hili kama mauaji ya halaiki kulingana na ushahidi wa kutosha, msingi wa kisheria ulio wazi na vigezo maalum. Rais wa Ufaransa amesema Paris inalitambua taifa huru la Palestina na kuwa suala hilo ni muhimu katika kusitisha vita dhidi ya Gaza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer pia ametangaza kuwa nchi hiyo inatambua rasmi Palestina ili kurejesha matumaini ya amani. Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney pia ametangaza uamuzi wa Ottawa wa kutambua taifa huru la Palestina. Undumakuwili wa misimamo ya nchi za Magharibi kuhusu kutambuliwa rasmi taifa la Palestina unasababishwa na msururu wa masuala ya kisiasa, kiuchumi, kihistoria na kidiplomasia. Nchi nyingi za Magharibi hususan Marekani zina uhusiano wa karibu wa kiusalama, kijeshi na kiuchumi na utawala wa Kizayuni.

Marekani na katika nchi nyingi za Ulaya, maoni ya umma yanaunga mkono Palestina, haswa baada ya mauaji ya kimbari huko Gaza. Serikali za Marekani na Magharibi mara nyingi huchukua misimamo ya kinembo tu kwa ajili ya kupunguza mashinikizo haya na kujaribu kuonyesha kwamba zinatetea haki za binadamu, lakini kwa kweli hakuna lolote la maana linalofanyika katika uwanja huo. Huko Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, lobi zenye nguvu zinazounga mkono Wazayuni zina taathira kubwa katika maamuzi ya sera za kigeni za nchi hizo. Lobi hizo huzizuia kuchukua misimamo iliyo wazi katika kuunga mkono Palestina.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

Kwa mujibu wa wachambuzi na taasisi nyingi zinazojitegemea, misimamo ya Marekani na nchi za Magharibi kuhusiana na vita vya Gaza si ya kuaminika wala iliyo na uwazi, jambo ambalo linadhihirika wazi sio tu katika hotuba za viongozi bali pia katika mienendo yao ya kisiasa na kidiplomasia. Kwa upande mmoja, nchi za Magharibi zinalaani jinai za utawala wa Kizayuni, lakini kwa upande mwingine zinaendelea kutoa misaada ya kifedha na kijeshi kwa utawala huo.

Marekani imepiga kura ya turufu mara kwa mara dhidi ya maazimio ya Baraza la Usalama yanayotaka kusitisha mapigano au kutuma misaada ya kibinadamu huko Gaza, huku ikidai kutetea haki za binadamu. Waitifaki wa Magharibi wa utawala wa Kizayuni ikiwemo Marekani wanazungumzia haki ya kujilinda utawala wa Kizayuni, katika hali ambayo utawala huo ghasibu hauna haki yoyote katika uwanja huo, kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Uungaji mkono usio na masharti kwa utawala wa Kizayuni umepoteza kabisa itibari ya Wamagharibi kuhusiana na madai yao ya eti ya kutetea haki za binadamu na hivyo kuibua hasira ya jamii ya kimataifa.

Nchi za Magharibi huku zikidai kuwa zinaunga mkono Wapalestina na wakaazi wa Gaza, katika miezi ya hivi karibuni zimetumia kila njia kuzuia kufichuliwa ukweli kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni. Hujuma za nchi za Magharibi katika vita vya Gaza zina mwelekeo mpana sana. Tokea kukwamisha uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu hadi kuvuruga usitishaji vita, hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kufikia malengo maovu ya utawala wa Kizayuni.

Kila mikutano ya taasisi za kimataifa kuanzia Baraza la Usalama hadi Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu imekuwa ikiambatana na uvurugaji wa Marekani na washirika wake wa Magharibi kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. Katika mikutano kadhaa ya Baraza la Usalama, Marekani imezuia na kupinga maazimio kuhusu vita vya Gaza, ikidai kwamba hatua yoyote kuhusu usitishaji vita inaweza kuimarisha Hamas.

Kwa upande mmoja, Marekani na serikali za Magharibi zinadai kuwa waungaji mkono wa watu wa Gaza, lakini nyuma ya pazia, zinatia saini mikataba ya silaha na utawala wa Kizayuni, kuupa misaada ya kila aina, na viongozi wao hufanya safari za mara kwa mara katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kukutana na baraza la mawaziri la utawala huo katili.

Katika hali ambayo Marekani na nchi za Magharibi na hasa waitifaki wa Ulaya wa Ikulu ya Marekani zinaendelea kuunga mkono utawala wa Kizayuni, suala la kutambuliwa taifa huru la Palestina ni mbinu ya kipropaganda tu inayolenga kupunguza mashinikizo na maoni ya waliowengi kimataifa. Wapigania uhuru na waungaji mkono wa Palestina kamwe hawatakubali misimamo na maonyesho ya kipropaganda ya watawala wa Magharibi kuhusu Palestina, kwa sababu serikali hizo ni washirika wakuu katika jinai za Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.

[ad_2]

BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *