Brigedi za al Qassam, tawi ila kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kuwa
vita yoyote dhidi ya Iran ni sawa na shambulio dhidi ya Umma mzima wa Kiislamu.

Abu Obeida Msemaji wa Brigedi za al Qassam ametangaza uungaji mkono wao kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa wananchi na serikali ya Iran kupitia taarifa yao ya jana wakati Iran ilipoadhimisha kutimia mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kushtadi vitisho vya  Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Abu Obeida amesema: ” Tuuhesabu uchokozi wowote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na watu wake kuwa uchokozi dhidi ya taifa letu la Kiislamu, na sawa na kukiuka mamkala ya kujitawala ya taifa la Kiislamu linaloendesha mapambano.

Wakati huo huo Abu Obeida amesema, wana imani na uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Iran likiwemo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC katika kukabiliana na hujuma yoyote, kuihami nchi hii na kutoa kipigo kikali kwa wavamizi.

Amesema, vikosi vya ulinzi vya Iran vimetoa somo kwa adui Mzayuni wakati wa hujuma haramu ya vita vya  siku 12  vya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwaka jana. 

Msemaji wa al Qassam amesema” Harakati ya Hamas iliweza kutoa kipigo kwa Wazayuni wakati wa Oparesheni ya Kimbunga cha al  Aqsa ya Oktoba 7, 2023 iliyofanywa kulipiza kisasi jinai kubwa za kila uchao za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.  

Kufuatia operesheni hiyo ya kihistoria ya Palestina, Israeli ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, lakini ilishindwa kufikia malengo yake yaliyotangazwa licha ya kuwaua sahidi Wapalestina wasiopungua 72,045, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 171,686.

Utawala mtenda jinai wa Israel ulilazimika kukubali kusitisha mapigano na Hamas; makubaliano ambayo yalianza kutekelezwa rasmi Oktoba 10 mwaka jana. Tangu wakati huo Israel karibu kila siku inakiuka makubaliano hayo kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Gaza. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *