Mkurugenzi wa Akili Education, Felician Chizelema, amesema kuwa wapo katika maandalizi ya mbio ndefu za Akili Alumni Marathon 2026 yanalenga kuweka rekodi ya dunia kwa kukusanya washiriki kutoka mataifa mengi zaidi duniani, angalau mshiriki mmoja kutoka kila nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Chizelema amesema kuwa kwa sasa marathon kubwa duniani zimewahi kukusanya washiriki kutoka mataifa 120 hadi 140, lakini hakuna iliyowahi kufikia uwakilishi wa karibu mataifa yote duniani na kwamba, endapo lengo hilo litafanikiwa, Tanzania itaingia kwenye historia ya Guinness World Record kwa mara ya kwanza kupitia mbio hizo.
Mbio hizo zinalenga kukusanya dola za Marekani milioni 1.2 ili kufadhili wanafunzi 100 kusoma kozi za teknolojia zenye mahitaji makubwa duniani, ikiwemo Cyber Security, Artificial Intelligence na Blockchain Technology.
Mgeni Rasmi kwenye mbio hizo anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVSports

(Feed generated with FetchRSS)