
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewasifu na kuwapongeza wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi kote nchini katika maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa maandamano hayo yamewakatisha tamaa maadui.
Ayatollah Khamenei alisema jana katika ujumbe wake kwa njia ya televisheni kwa wananchi wa Iran kwamba:” Tarehe 22 Bahman (Februari 11) mwaka huu, mmetekeleza jambo kubwa; mmeiletea heshima Iran.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika ujumbe wake huo kwamba: ” Kama kawaida mmeizidishia nguvu Jamhuri ya Kiislamu kwa uungaji mkono wenu wa siku zote; na maadui ambao walitala kusalimu amri taifa hili wamekata tamaa katika kauli na mipango yao.”
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ameyataja malipo ya harakati hiyo kubwa ya umma kuwa ni heshima ya hali ya juu, mamlaka yenye nguvu zaidi na uhuru kamili zaidi wa Iran na kuongeza kuwa: “Sote tujitahidi kuulinda uhusiano huu na mafungamano ya kitaifa ambayo ni ya thamani kubwa.”
Ayatullah Khamenei amepongeza ushiriki wa wananchi na kujitokeza kwa hamasd kubwa katika mitaa mbalimbali ya Iran huku wakipiga nara kwa umoja na kusema wananchi wa Iran katika maandamano ya 22 Bahman wamedhihirisha utambulisho na mwenendo wao kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.
Ayatullah Khamenei amesema analishukuru taifa zima la Iran na snatuma salamu kwa kila mwananchi sliyrdhiriki katika mkusanyiko huo uliowakutanisha pakubwa mamilioni ya wananchi wa Iran kote nchini.
Makumi ya mamilioni ya Wairani walimiminika mitaani kote nchini siku ya Jumatano, kuadhimisha mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuwa miongoni mwa mahudhurio makubwa zaidi ya kitaifa kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.