#HABARI: Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mkakati wa kuongeza fani mpya katika Chuo cha VETA mkoani Kagera zitakazosaidia kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na rasilimali nyingine za mkoa huo.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA, Dkt. Abdallah Ngodu, amebainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuwapa vijana ujuzi wa kisasa utakaopanua wigo wa kujiajiri na kuajiriwa, akizungumza wakati wa ziara ya Baraza la Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika chuo cha VETA Burugo wilayani Bukoba.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki, Kosamu Joseph, ameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kuwaandaa vijana kupitia mafunzo ya amali ili kukabiliana na changamoto za soko la ajira.

Wanafunzi wa chuo hicho wameeleza kuwa ujuzi wanaoupata unawapa ujasiri wa kujitegemea kiuchumi, jambo litakalosaidia kuinua kipato chao na kuchochea maendeleo ya rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *