‎#MICHEZO: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amewasili rasmi nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho hilo.

‎Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, Terminal 1, jijini Dar es Salaam.

‎Dkt. Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

‎Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.

‎Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *