Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kumtusi Rais wa utawala wa kizayuni wa Israel akimuunga mkono waziri mkuu wa utawala huo yameongeza mvutano kati ya Netanyahu na Isaac Herzog.

Kufuatia kauli kali za Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Rais wa Israel Isaac Herzog, mvutano usio wa kawaida umeibuka kati yake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeripoti kwamba Herzog anasubiri maelezo ya Netanyahu. Anataka kujua kama uchochezi wa Netanyahu ndio uliosababisha “kauli hizi za kijeuri” ambazo zimeleta pigo kubwa kwa nafasi ya mamlaka ya utawala wa Kizayuni.

Gazeti hilo, likinukuu vyanzo vilivyo karibu na Herzog, liliandika kwamba ikiwa itabainika kwamba Netanyahu ndiye aliyesababisha matamshi haya na kwamba alimkasirisha Trump, itathibitika kwamba alivuka mstari mwekundu.

Gazeti hilo liliongeza: “Kuna tofauti kati ya ukosoaji na matusi, na matamshi ya Trump yalikuwa matusi.”

Kuhusiana na hili, wale walio karibu na rais wa Israel wamesema: “Tunataka kujua kama Netanyahu alihusika katika jambo hili na kama alimtaka Trump kutoa matamshi makali kama hayo dhidi ya Herzog.”

Siku moja tu baada ya kukutana na Netanyahu huko Washington, Trump alianzisha shambulio lisilo la kawaida dhidi ya Herzog, akisema kwamba Herzog anapaswa kuona aibu kwa kutomsamehe Netanyahu.

Trump aliongeza: “Netanyahu alikuwa waziri mkuu mzuri wakati wa vita. Alikuwa hodari sana na tulifanya naye kazi vizuri.”

Aliongeza: “Kama unavyojua, kuna rais huko Israel ambaye anakataa kumsamehe Netanyahu katika kesi ya sasa. Nadhani hii ni aibu na fedheha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *