
Dar es Salaam. Yas imewaaga rasmi wateja wake 10 wanaosafiri kwenda Dubai baada ya kushinda kupitia kampeni ya ‘Tunasheherekea Pamoja – Mwaka Mmoja wa Yas’.
Hafla ya kuwaaga washindi hao, imefanyika leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Dar Kaskazini, Aidan Komba, alisema safari hiyo ni ishara ya kuthamini wateja ambao wameendelea kuiunga mkono Yas katika kipindi chote cha ukuaji wake ndani ya mwaka mmoja.
Alibainisha kuwa mabadiliko ya chapa yameenda sambamba na maboresho ya huduma, upanuzi wa mtandao na ushiriki mpana zaidi wa wateja kote nchini.
Kampeni hiyo, ambayo ilianza tarehe 23 Januari, imeshakabidhi zawadi kwa zaidi ya wateja 70 wakiwemo waliojinyakulia fedha taslimu, simu janja na router za 5G.
Kwa mujibu wa Komba, zawadi hizo ni sehemu ya kurudisha shukran kwa wateja wa Yas na kutambua mchango wao katika ustawi wa chapa hiyo.
Komba aliongeza kuwa kampeni imeimarisha uhusiano kati ya Kampuni na wateja wake huku ikihamasisha matumizi ya huduma za kidijitali na uwezeshaji kwa watanzania.
Kampeni hiyo inakwenda sambamba na juhudi za kuendelea kupanua na kuboresha huduma za 4G na 5G ili kukidhi mahitaji ya kasi na nguvu ya mtandao.
Aliwapongeza washindi wote 10, akisema wanaibeba chapa ya Yas wanapoanza safari hiyo. Aidha, alikumbusha kuwa kampeni bado inaendelea na kuwataka wateja waendelee kushiriki kupitia matumizi ya huduma mbalimbali za Yas kama vifurushi vya sauti, data, intaneti na bidhaa zingine. Alisema kampeni itahitimishwa kwa utoaji wa zawadi kubwa ya shilingi milioni 100.
Mmoja wa washindi, Violeth Lema kutoka Arusha, alisema, Safari hiyo ya bure anaichukulia kuwa moja ya njia nzuri ya kuwaunganisha wateja wa kutoka maeneo mbalimbali kwenda kufurahi pamoja. Akizungumza na wanahabari alisema alipopigiwa simu kutoka huduma kutoka huduma kwa wateja ilibaki kidogo tu apuuzie simu hiyo ambayo ilimpa taarifa nzuri za ushindi wake wa safari ya Dubai.
“Nilipoona namba 100 mara ya kwanza, nilisita kupokea. Nilidhani ni simu ya kawaida tu. Lakini nilipopokea, nikaambiwa ni mmoja wa washindi. Nilifurahi sana, sikuamini kabisa,” na kuongeza kwa kuishukuru mtandao huo kwa kuja na Kampeni nzuri kwa ajili ya wateja wake.