#HABARI: Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika, umeteketeza nyumba ya familia moja katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo mama aliyekuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo amefanikiwa kunusurika kifo na kuokoa baadhi ya vyombo vyake, huku mali nyingine zikiharibiwa vibaya na moto uliokuwa ukisambaa kwa kasi.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefika eneo la tukio na kufanya jitihada kubwa za kuuzima moto huo ili kuzuia usisambae kwenye nyumba za majirani na kuleta madhara zaidi.
Wakati harakati za uokoaji zikiendelea, taharuki imetanda kwa wakazi wa eneo hilo, huku mamlaka zikitarajiwa kuanza uchunguzi rasmi kubaini chanzo cha janga hilo na thamani ya mali zilizopotea.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.