#HABARI: Wafadhili wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia, wamewasili nchini na kutembelea utekelezaji wa mradi huo jijini Arusha kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, mwakilishi wa Benki ya Dunia Paul Seadkwa, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo, huku akibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto chache, Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha mradi unakamilika na malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.

Kwa upande wao wasimamizi wa mradi huo akiwemo Bakari Mwamgugu, Dkt. Angelina Mussa, pamoja na Lali Hamis Ali kutoka Zanzibar, wamesema mradi ulioanza mwaka 2021 unatarajiwa kukamilika mwaka 2026 na tayari umeanza kuleta matokeo chanya.

Wamesema hadi sasa minara 758 ya mawasiliano imejengwa Tanzania Bara na Zanzibar, huku ofisi 851 za Serikali zikiwa tayari zimeunganishwa kwenye mkongo wa taifa.

Wameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha Tanzania kujenga jamii yenye uwezo mkubwa wa matumizi ya teknolojia ya kidijitali na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *