#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Geofrey Timoth, amesema kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ametenga Shilingi milioni 17.5 kwa ajili ya ujenzi wa kivuli, huku akisisitiza kuwa kazi hiyo ianze mara moja kwa kuwa fedha tayari zipo.
Timoth alisema Kamati ya Maendeleo ya Jimbo imeridhia eneo hilo kujengwa kivuli ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na wananchi.
Alitoa maelekezo kwa Afisa Biashara na Mhandisi anayesimamia mradi huo kuhakikisha ujenzi unatekelezwa kwa haraka.
Kuhusu mikopo ya asilimia 10, mbunge huyo alisema anataka kuona wananchi wengi zaidi wakinufaika na mpango huo, akibainisha kuwa Serikali imetenga Shilingi bilioni 200 kwa ajili ya mikopo hiyo nchi nzima.
Amewasisitiza wote wanaohusika na utoaji wa mikopo ndani ya jimbo hilo kuhakikisha wanarahisisha upatikanaji wake kwa wananchi wenye uhitaji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Timoth aliyasema hayo leo Jumanne, Februari 17, 2026, wakati wa ziara ya kukagua miradi itakayofadhiliwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la Kawe kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.