s

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Katika siku za hivi karibuni, visa vya kurekodiwa kwa siri vimeibua hofu kubwa miongoni mwa wanawake na wasichana barani Afrika. Kenya na Ghana ni mfano wa hili kutokana na kisa cha raia wa Urusi ambaye alidaiwa kurekodi wanawake bila idhini yao, kisha kuchapishwa video hizo mtandaoni.

Tukio hili linaonyesha jinsi teknolojia ya kisasa inaweza kutumika vibaya, ikiathiri faragha na usalama wa mtu binafsi. Kwa wengi, kisa hiki limefunua hatari ambazo hazikuonekana hapo awali katika maisha ya kila siku.

Kamera za siri kwenye miwani, kalamu, vyumbani na maeneo mengine kwa sasa zimekuwa hatari kwa faragha za wengi. China imeripotiwa aina hii ya matukio mengi kama ilivyo kwa nchi zingine Ulaya na Asia.

Tukio hili la Kenya na Ghana limeibua mjadala mkubwa kuhusu ulinzi wa wanawake na wasichana, na nguvu ya kisheria katika kukabiliana na teknolojia mpya. Kenya chini ya Computer Misuse and Cybercrimes Act 2018 inatoa adhabu ya kufungwa hadi miaka miwili kwa mtu anayechapisha picha au video za mtu mwingine bila idhini.

Ghana, kwa upande wake, imeanzisha sheria kali chini ya Cybersecurity Act 2020, ikitaja adhabu ya hadi miaka 25 kwa wale wanaochapisha video au picha bila idhini, hasa za wanawake na watoto.

Kilichotokea Kenya na Ghana

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Kenya na Ghana zimejikuta zikiwa kwenye vichwa vya habari baada ya kijana Mrusi, anayejulikana kama Yaytseslav, kurekodi wanawake bila idhini yao. Kwa mujibu wa taarifa, yeye alitumia miwani yenye kamera ya siri kurekodi video za wanawake wakati wa mazungumzo yao au na mengine ya faragha, kisha kuchapisha video hizo kwenye mitandao ya kijamii bila ridhaa. Visa hivi vimeibua taharuki kubwa miongoni mwa wanawake, huku wengi wakilalamika kuingiliwa faragha yao.

Serikali ya Kenya ilitoa taarifa rasmi ikisema kwamba vyombo vya usalama vimeagizwa kuchunguza tukio hili mara moja. Waziri wa Jinsia Hanna Cheptumo alilaani vitendo hivi akisema kuwa ni unyanyasaji wa kijinsia unaotekelezwa kwa kutumia teknolojia na kwamba serikali itachukua hatua kali kuhakikisha wahusika wanakabiliwa na sheria.

Ghana pia imechukua hatua za kisheria, ikisema inakusudia kuomba Urusi imruhusu kijana huyo kupelekwa Ghana ili akabiliwe na sheria. Waziri wa Teknolojia Sam George alisisitiza kuwa nchi yake itatumia rasilimali zote zilizopo, ikiwemo kushirikiana na Interpol na maofisa wa Urusi, kuhakikisha wahusika wanawajibika. Hata hivyo, Urusi haikuthibitisha wazi ikiwa itashirikiana na uchunguzi wa Ghana, jambo linaloongeza changamoto ya kisheria.

Waziri huyo, amesema kwamba mawasiliano na balozi wa Kirusi yameshafanyika ili kushirikiana katika kufuata kesi hii, ingawa Urusi ina sera ya kutorudisha raia wake, inaweza kufanya hivyo katika mazingira ya dharura.

Kenya chini ya sheria ya Computer Misuse and Cybercrimes Act 2018 inatoa adhabu ya kufungwa hadi miaka miwili kwa mtu anayechapisha picha au video za mtu mwingine bila idhini. Ghana, kwa upande wake, imeanzisha sheria kali chini ya Cybersecurity Act 2020, ikitaja adhabu ya hadi miaka 25 kwa wale wanaoshiriki video au picha zisizo na idhini, hasa za wanawake na watoto.

Namna kamera za siri zinavyofanya kazi

Miwani yenye kamera ni mojawapo ya teknolojia zinazotumika kurekodi kwa siri. Kamera ndogo huwekwa ndani ya fremu ya miwani, mara nyingi katikati au upande wa pembeni, kurekodi video au picha bila mtu kujua. Baadhi ya miwani hii huja na betri inayochajiwa kupitia USB, na inaruhusu kurekodi kwa dakika 60 hadi 90 kulingana na aina ya miwani.

Sehemu ya kumbukumbu, kama microSD, huhifadhi video na picha moja kwa moja. Miwani hii nyingi kupitia sehemu ya kuwashia na kuzimia “Power” unaweza kurekodi na kusitisha kurekodi.

Baadhi ya aina zina vitu vya ziada kama Bluetooth kwa mawasiliano au muziki, maiki kwa ajili ya kurekodi sauti, na lenzi ‘polarized lenses’ kwa ajili ya jua.

Kwa wale wanaotumia teknolojia hii, mtazamo wa macho na fremu ndogo huwezesha kurekodi mtu bila yeye kujua. Hii ni sababu kuu kwa nini visa vya Kenya na Ghana vilikuwa na mvuto mkubwa mtandaoni, huku wahusika wakipata udhalilishaji mkubwa wa faragha.

Namna ya kujilinda usirekodiwa kwa siri

Kuna mbinu mbalimbali zinazoweza kusaidia mtu kujiulinda dhidi ya kamera za siri. Kwanza, kutumia simu kupitia Guided Access na Accessibility Shortcut, pamoja na kuchagua Magnifier, inaweza kusaidia kugundua kamera zilizofichwa ndani ya chumba.

Bonyeza mara tatu kwenye sehemu za kuzimia husaidia kugundua vifaa vya ‘elektroniki vilivyojificha kama kamera za simu, kamera za miwani na nyingine utakapokuwa mazingira ya ndani.

Pili, ni muhimu kuwa makini na mazingira unayokuwa. Vyumba vya hoteli, ofisi ndogo, au vyumba vya kubadilisha nguo vinaweza kuwa na kamera. Angalia nyuso zisizo za kawaida, vifaa vinavyobadilika mara kwa mara, na vitu vya elektroniki visivyojulikana. Mbinu hii husaidia kupunguza hatari ya kurekodiwa bila ridhaa.

Tatu, angalia vitaa, au kitaa kinachowakawaka, kamera nyingi za kificho zina aina hii za taa ambazo kwa macho ya haraka haraka huwezi kuona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *