Picha iliyochukuliwa kutokea angani inayoonyesha mazishi ya wanafunzi 168 waliouawa shahidi wakati wa shambulio la makombora ya Marekani dhidi ya Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab, kusini mwa Iran, imeshinda tuzo ya juu katika Kategoria ya Upigaji Picha za Habari ya tuzo za Golden Shot Photography Awards 2026.

Morteza Akhondi, mpiga picha kutoka mkoa wa Hormozgan, ameshika nafasi ya kwanza katika shindano la kimataifa kwa picha yake ya kuvutia, ambayo imeathiri maoni ya majaji wa kimataifa.

Katika orodha ya mwisho ya mashindano hayo, Akhondi kutoka Iran ametwaa medali ya dhahabu, akifuatiwa na Bartosz Matenko wa Poland katika nafasi ya pili na Mohammad Mohtaseb wa Saudi Arabia katika nafasi ya tatu.

Muungano wa kijeshi wa Marekani na Israel uliishambulia Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab mnamo Februari 28, katika siku ya kwanza kabisa ya uchokozi wa tawala hizo mbili dhidi ya Iran.

Shule hiyo ilishambuliwa mara matatu tofauti kwa kutumia makombora ya Tomahawk—yaliyotengenezwa na Raytheon huko Tucson, Arizona nchini Marekani.

Wanafunzi 168 na walimu 26 wa kike waliuawa kinyama katika mashambulizi hayo, na zaidi ya watu 95 walijeruhiwa. Waathiriwa wengi walikuwa wasichana na wavulana wenye umri wa kati ya miaka saba na kumi na miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *