Wachambuzi wa soka @akingamkono na @rashidy_hamis wameunga mkono kauli ya Kocha wa Coastal Union, Mohamed Muya, aliyesema bado hajaridhishwa na ufanisi wa safu ya ushambuliaji ya timu yake licha ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nyumbu FC.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Muya alisema timu yake ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini ilishindwa kuzitumia ipasavyo, jambo alilodai linahitaji kufanyiwa kazi kabla ya michezo ijayo.
Akichambua kauli hiyo, @akingamkono amesema ni kawaida kwa kocha kuangalia zaidi mapungufu hata baada ya ushindi, hasa pale timu inapokosa umakini katika kumalizia mashambulizi.
Kwa upande wake, @rashidy_hamis amesema kocha Muya yupo sahihi, akieleza kuwa mbinu za mashambulizi ya haraka anazotumia zinaiwezesha Coastal kufika mara kwa mara langoni kwa wapinzani, hivyo ni muhimu kwa washambuliaji kuongeza umakini ili kubadilisha nafasi hizo kuwa mabao.
#viwanjani
(Feed generated with FetchRSS)