HABARI: Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza kuchukua hatua ya kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyo rasmi.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo.

“Inawezekana lisiwe jambo zuri na yanaweza kuwa maelekezo machungu kwa wafanyabiashara, lakini huwezi kujenga nyumba yenye thamani ukaziba barabara. Naamini diplomasia itaendelea kutumika pasipo kutumia nguvu kwamba barabara zitabaki wazi,” amesema RC.

Akizungumza katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chalamila amesema kuanza kwa huduma katika Soko Kuu la Kariakoo kutaambatana na kufunguliwa kwa barabara zote zinazoingia na kutoka sokoni humo.

Februari 17, 2026 Jana, Jumanne , katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo, kulikuwa kumebandikwa matangazo yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, akiwataka wafanyabiashara wanaopanga na kuuza bidhaa katikati ya barabara za mitaa na njia za waenda kwa miguu ambao hawajapangwa waondoe bidhaa zao mara moja.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *