MOROGORO: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefanikiwa kutatua migogoro ya mipaka 423 kati ya 438 iliyokuwa inahusiana na vijiji na Wadau wengine iliyoanishwa kupitia lamati ya mawaziri wanane iliyoundwa na hivyo kusalia migogoro 15.

Kamisha wa Uhifadhi wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema hayo kwenye taarifa yake mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande kabla ya kufungua mkutano wa nne wa Makamanda, maofisa na askari uliofanyika mjini Morogoro.

Profesa Silayo amesema chini ya maelekezo ya Rais kupitia Kamati ya Mawaziri nane katika kipindi cha hivi karibuni imeweza kutatua migogoro mingi Kwa kiwango Cha asilimia 96 iliyokuwa inaikabili misitu yetu.

Kamishna wa Uhifadhi wa TFS alisema Katika kutekeleza maelekezo hayo na yale yaliyotiolewa wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri Wakala ulihakikisha maeneo ambayo migogoro imetatuliwa, uvamizi wa misitu au migogoro mipya haijitokezi tena.

“Tutahakikisha kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine tunamaliza kabisa utatuzi wa migogoro 15 iliyobakia na juhudi zinaendelea kuimaliza,” amesema Profesa Silayo.

Akifungua mkutano huo ,Naibu Wizara ya Maliasili na Utalii ,Chande ameutaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuongeza kiwango cha uzalishaji wa asali kutoka tani 9.5 inayouzwa nje ya nchi kwa mwaka na kufikish tani 50,000 Kwa mwaka.

” Kiwango hiki kinaweza kuongezeka endapo Wakala kupitia Wataalamu waliopo watatumia rasilimali za misitu kwa kuwa Kuna makundi ya nyuki Zaidi ya milioni tisa”amesema Chande.

Chande amesema asali ya Tanzania imepata soko kubwa nchi za nje kutokana na ubora wake ,hivyo Wakala unapaswa kuongeza juhudi katika kuongeza uzalishaji ili kuongeza kiwango cha mauzo ya nje na kuingiza fedha za kutoka kwa wakala na Serikali.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFS, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amesema Bodi itaendela kusimamia utekelezaji wa maamuI na kutoa ushauri wa kitaalam Ili kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro Kwa la Kuzuia Changamoto hizo kutojitomeza siku zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *