Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa kampuni kubwa ya teknolojia ya Meta, zamani facebook, Mark Zuckerberg, amekuwa Mahakamani jijini Los Angeles nchini Marekani, kujibu tuhuma kuhusu namna matumizi ya mtandao hasa wa Instagram, unavyoathiri afya ya akili kwa watoto na vijana nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Zuckerberg, amejitetea kuhusu madai ya kuwa matumizi ya Instagram, kwa vijana na watoto nchini Marekani, imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa magonjwa ya akili nchini Marekani.

Mtumiaji mmoja Mark Lanier, amekwenda Mahakamani kuishtaki kampuni hiyo baada ya matumizi ya Instagram na Youtube kumsabababishia ugonjwa wa akili alipokuwa mdogo.

Mwanamke huyo anasema, mitandao hiyo miwili, ilimfanya kuwa na mawazo ya kujitoa uhai, lakini pia kupata msongo mkubwa wa mawazo.

Mmiliki wa kampuni ya Meta Mark Zuckerberg
Mmiliki wa kampuni ya Meta Mark Zuckerberg REUTERS – Mike Blake

Zuckerberg, anashtumiwa kwa kulipotosha bunge la Congress mwaka 2024 kwamba, muundo wa mitandao yake ya kijamii, haina athari kwa watuamiaji.

Iwapo mmiliki wa kampuni hiyo atapoteza kesi hiyo, atawalipa fidia kwa wale wote waliothrika na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Katika hatua nyingine,  kesi nyingine zaidi ya 1,600 zimefunguliwa nchini Marekani dhidi ya  matumizi mengine ya mitandao ya kijamiii kama Tiktok, Google na Snap ambayo ripoti zinasema, inasababisha magonjwa ya akili hasa kwa vijana na watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *