Dar es Salaam. Kombinesheni ya msanii wa bongo fleva, Sarah Michael ‘Phina’ na Eni, raia wa Nigeria, inazidi kuwaunganisha na mashabiki wanaozifuatilia kazi zao. Baada ya mastaa hao kuamua kutoa zawadi kwa atakayefanya chalenji nzuri ya wimbo wao wa Nakuamini.

Wimbo wa Nakuamini waliutoa kabla ya Valentine’s Day Februari 14, ulitrendi katika mtandao wa TikTok kwa watu kufanya chalenji ya kuonyesha upendo, jambo lililowaibua mastaa hao kutangaza zawadi.

Phina na Eni walitangaza mashabiki watengeneze video kali kuanzia Februari hadi Machi 17 na itakayofanya vizuri mshindi wa kwanza atapata Sh1 milioni, wa pili Sh.750,000 na mshindi wa tatu atapata Sh500,000, kitu kilichowafurahisha zaidi mashabiki kuona wanathaminiwa.

Phina amesema wanatoa fursa kwa mashabiki wao, ili kupata pesa pia inawapa fursa ya kuonekana kwa kile wanachokifanya.

“Nilichojifunza katika soko la nje la muziki, kuna uwekezaji mkubwa wa pesa ambao wenzetu wanaufanya. Hilo linawafanya wapate nafasi ya kuonekana katika majukwaa makubwa ya kimataifa,” amesema Phina na kuongeza;

“Mashabiki wetu wamekuwa wakitupokea vizuri katika kazi tunazozitoa na tutaendelea kufanya vitu bora zaidi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *